Saturday, January 30, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA KUSHIRIKI IBADA YA ASKOFU MKUU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHELI TANZANIA (KKKT) MJINI MOSHI.

IMG_4361 (1024x683)Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.
IMG_4355 (1024x683)
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozung4umza nao ofisini kwake.
……………………………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada maalum ya kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi mjini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema waziri mkuu anatarajiwa kuwasili mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya shughuli za kanisa.
Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri yeyote wa serikali ya awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo maalum atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.
Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi wa madhehebu tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na wananchi kwa ujumla.
Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa mkoa,aliwataka wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa
Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa maelekezo ya serikali kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa taarifa ya mkoa.
Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Kaskazini amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.
Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti mwaka jana katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.
Uchaguzi wa nafasi hiyo uliwashindanisha askofu Dk Stephen Munga wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema wa dayosisi ya Pare.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

.
.
.. .
DSC00529
.

.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC00558
.
DSC00560
.
DSC00563
.
DSC00566
.
DSC00569
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.
 WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther (kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
 DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
 Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.

WATENDAJI SABA WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI WA MILIONI 851 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA

Na Faustine Ruta, Bukoba.

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera limewasimamisha kazi Watendaji sita wa Halmashauri kupisha uchunguzi wa upotevu na ubadhirifu wa milioni 851 za mfuko wa barabara, Mfuko wa Afya, na Mfuko wa Jimbo zilizotumika bila kufuata utaratibu na kanuni za fedha. 

Watendaji hao sita waliosimamishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Januari 28 mwaka huu walihusika na ubadhilifu wa fedha hizo kwa kuzitumia bila kufuata kanuni, taratibu na sheria za kuomba idhini ya kuhamisha vifungu vya fedha au kubadilisha matumizi yake kutoka fungu moja kwenda fungu lingine. 
Hayo yalibainishwa na Kamati ya Wataalamu sita iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mongella katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika tarehe 21.01.2016 Mkoani Kagera na kuiagiza Kamati hiyo kuchunguza upotevu wa fedha hizo mara baada ya Mhandisi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2014/2015. 
Kamati hiyo ya wajumbe sita iliyoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera Bw. Sabora Wambura na ilipewa siku tano iwe imekamilisha taarifa yake. Aidha, taarifa ya Kamati hiyo iliwasilishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa, Baraza la Madiwani, Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Kamati ya Ulinzi na Usalaama ya Mkoa na Wilaya Januari 27 mwaka huu. 

Katika kikao hicho cha kupokea taarifa ya ubadhirifu wa shilingi milioni 851, Watendaji waliohusika walihojiwa mara baada ya taarifa kuwasilishwa na kuonekana walitumia fedha hizo kinyume na utaratibu wa fedha, katika mahojiano hayo walikiri kuwa utaratibu wa fedha haukufuatwa na kukiri makosa yao. 
Mkuu wa Mkoa Mhe. Mongella mara baada ya kuwahoji alikubaliana na Baraza la Madiwani kuwa watendaji hao wanatakiwa kuwajibishwa na kuliagiza Baraza hilo kukaa kikao na kuamua hatua ya kuchukua kwa wahusika wote kwani mamlaka ya kuwawajibisha Wakuu wa Idara wa halmashauri ipo kwa Madiwani wenyewe. 

Aidha, alimwagiza Katibu Tawala Mkoa kumwadikia barua Katibu Mkuu TAMISEMI ili aweze kumchukulia hatua Mkurugenzi Mtendaji Bi Gradis Dyamvunye aliyekuwepo wakati huo na kuomba aliyekuwa Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo Robert Massoro kurudishwa kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa barabara pia kuomba ufanyike ukaguzi maalum mara moaja. 

Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Januari 28 mwaka huu kikiongozwa na Mwenyekiti wake Mustapha Ngeze kiliamua kwa kauli moja kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi wa upotevu wa milioni 851 watendaji wafuatao; 

Idara ya fedha ni Bw. Jonathan Katunzi (Mweka Hazina), Selialisi Mutalemwa, Idara ya Ujenzi, Bw. Deus Bizibu, Elimu Sekondari ni Bw. Lucas Mzungu, Mifugo ni Dk. Kisanga Makigo na Bw.Mustapha Sabuni Afisa Mipango. 
Mchanganuo wa fedha zilizotumika blia kufuata utaratibu na kanuni za fedha ni Shilingi milioni 200 za mfuko maalum wa barabara zilizokuwa zimeletwa kwa ajili ya kujenga daraja la Kyamabale, Milioni 176 za mfuko wa barabara kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati barabara, Milioni 168 za mfuko wa Jimbo, na Milioni 307 za mfuko wa Afya (Busket Fund) 

UMOJA WA WANAWAKE TUGHE TAWI LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUTANA, WAJADILI UMOJA NA USHIRIKIANO JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PSPF YASAIDIA VITI KITUO CHA WALIMU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Francis Mselem, (kulia), akipena mikono na Mkuu wa Kituo cha Walimu, Mbagala, Bi.Fausta B.Luoga, wakati akimkabidhi msaada wa viti kwenye kituo hicho jijini Dar es Salaam leo Januari 29, 2016. Kituo hicho kinatumiwa na Walimu zaidi ya 1500, na wanafunzi 55. Wanaoshuhudia ni Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Bi. Coleta Mnyamani (wapili kushoto) na Balozi wa Mfuko huo, Bw. Mrisho Mpoto.
 Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, (kushoto), na Afisa Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Scola Mnyamani, wakiwasili kwenye kituo cha Walimu Mbagala jijini Dar es Salaam, Januari 29, 2016
 Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, na Afisa Masoko na Mahusiano wa Mfuko huo, wakiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbagala

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE LEO MJINI DODOMA

Baadhi ya wabunge wakiwasili katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Spika Mhe Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Adrew Chenge akiwakiwasilia tayari kuongoza kikao cha Bunge katika Bunge la 11 linaloendelea mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt Philip Mpango akiwasilisha hoja ya Serikali ili Bunge lijadili na kuidhinisha Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Suleiman Jafo akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe.Prof Joyce Ndalichako akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Naibu wake Mhe.Annastazia Wambura walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT) Mhe. Zitto Kabwe walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma