Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inatarajia
kupeleka kesi 36 mahakamani kwa tuhuma za kushiriki katika vitendo vya
rushwa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina Valentino Mlowola kuwa atafanya
kazi hiyo ikiwa ni dhamira ya Rais kuhakikisha mapambano dhidi ya rushwa
na ufisadi yanashughulikiwa bila kumuonea huruma
Amesema taasisi zitakazopelekwa Mahakamani ni Lake Oil katika kesi
ya ukwepaji kodi katika shauri linalohusu udanganyifu na ukwepaji
kodi.
Kamishina, Mlowola amesema kesi hiyo Lake Oil ilidanganya kwamba
lita za mafuta ya petrol 17,461,111,.54 zimesafirishwa kwenda nchini
Congo kupitia Zambia na kuisababishia hasara serikali sh.bilioni 8.5
wakati wa mafuta hayo yaliuzwa katika soko la ndani.
Kesi nyingine ni malipo ya dola za Marekani 6,000,000 ambazo
kampuni ya EGMA kwa madai kuwa malipo ya kampuni hiyo kwa kusaidia
Tanzania kupata mkopo dola za Kimarekani bilioni mia sita na
kutakatishwa na watumishi wa umma wasio waaminifu kwa kushirikiana na
baadhi ya watu wa sekta binafsiwakifahamu kuwa fedha hizo wamezipata kwa
njia haramu.
Kamishina Mlowola amesema baadhi ya watumishi wataofikishwa
mahakamani ni Shirika la Hodhi la Reli Nchini (RAHCO) kwa kukiuka kanuni
na taratibu za kuwapata wazabuni wenye ujenzi wa wa reli ya Kisasa ya
Kimataifa.
Katika Mlolongo kesi ni pamoja na kesi ya mabehewa ya Kokoto ya
Shirika la Reli Nchini katika ukiukwaji wa manunuzi wa mabehewa 25 ya
kokoto.
Aidha amesema kuwa kesi zote zimekamilika kwa uchunguzi na
wameshapeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini kuomba kibali cha
kuwafikisha mahakamani kwa wale wote waliobainika kujihusisha na matendo
ya rushwa na ukiukwaji wa sharia ,taratibu na Kanuni za manunuzi wa
Umma.
Amesema watumishi wa wa umma wafanye kazi kwa sheria na maadili
kwani Takukuru haitawavumilia watu wataohusika na rushwa katika
mazingira ya kazi.
Kamishina Mlowola amesema kuwa kazi alionayo ni kwenda sambamba na
Rais Magufuli dhidi ya mapambano ya rushwa na ufisadi kwenda kwa
vitendo bila ya kumuonea mtu.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
(Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola (kushoto), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari ofisini jijini Dar es Salaam leo asubuhi
kuhusu mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo ya kupambana na rushwa nchini
hasa kwa watendaji wa Umma na kesi zinazochunguzwa ili watuhumiwa
wafikishwe mahakama wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi
wake.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Kulia ni John David wa Gazeti la Majira.
Mwendeshaji wa Mtandao wa Fullshangwe, John Bukuku (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment