Mkuu
wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zalmira Rodrigues akizungumza
wakati wa kufunga kongamano la siku mbili Januari 27, 2016 jijini Dar es
Salaam kongamano hilo lilikuwa linajadili vipaumbele kwa miaka mitano
ijayo vinavyotakiwa katika kuandaa mpango ili kuhakikisha elimu ya
Tanzania inakua na ubora zaidi ambapo vipaumbele vimepitishwa ambavyo
vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa
miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
(HABARI PICHA-NA PHILEMON SOLOMON FULLSHANGWEBLOG)

………………………………………………………………………………….
Kongamano
lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) likisaidiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Mafunzo ya Ufundi limemalizika leo jijini Dar es Salaam baada ya
kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo waweze kujiajiri.
“Tumethibitisha yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,” alisema Tandari.
Aidha Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi wanataraji utendaji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
Nae Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zalmira Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika.
Awali Zalmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.

No comments:
Post a Comment