Baraza
la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera
limewasimamisha kazi Watendaji sita wa Halmashauri kupisha uchunguzi wa
upotevu na ubadhirifu wa milioni 851 za mfuko wa barabara, Mfuko wa
Afya, na Mfuko wa Jimbo zilizotumika bila kufuata utaratibu na kanuni za
fedha.
Watendaji
hao sita waliosimamishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha
Januari 28 mwaka huu walihusika na ubadhilifu wa fedha hizo kwa
kuzitumia bila kufuata kanuni, taratibu na sheria za kuomba idhini ya
kuhamisha vifungu vya fedha au kubadilisha matumizi yake kutoka fungu
moja kwenda fungu lingine.
Katika
kikao hicho cha kupokea taarifa ya ubadhirifu wa shilingi milioni 851,
Watendaji waliohusika walihojiwa mara baada ya taarifa kuwasilishwa na
kuonekana walitumia fedha hizo kinyume na utaratibu wa fedha, katika
mahojiano hayo walikiri kuwa utaratibu wa fedha haukufuatwa na kukiri
makosa yao.
Aidha,
alimwagiza Katibu Tawala Mkoa kumwadikia barua Katibu Mkuu TAMISEMI ili
aweze kumchukulia hatua Mkurugenzi Mtendaji Bi Gradis Dyamvunye
aliyekuwepo wakati huo na kuomba aliyekuwa Mhandisi wa Ujenzi wa
Halmashauri hiyo Robert Massoro kurudishwa kujibu tuhuma za matumizi
mabaya ya fedha za mfuko wa barabara pia kuomba ufanyike ukaguzi maalum
mara moaja.
Kikao
cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Januari 28 mwaka huu kikiongozwa
na Mwenyekiti wake Mustapha Ngeze kiliamua kwa kauli moja kuwasimamisha
kazi kupisha uchunguzi wa upotevu wa milioni 851 watendaji wafuatao;
Idara
ya fedha ni Bw. Jonathan Katunzi (Mweka Hazina), Selialisi Mutalemwa,
Idara ya Ujenzi, Bw. Deus Bizibu, Elimu Sekondari ni Bw. Lucas Mzungu,
Mifugo ni Dk. Kisanga Makigo na Bw.Mustapha Sabuni Afisa Mipango.
Mchanganuo
wa fedha zilizotumika blia kufuata utaratibu na kanuni za fedha ni
Shilingi milioni 200 za mfuko maalum wa barabara zilizokuwa zimeletwa
kwa ajili ya kujenga daraja la Kyamabale, Milioni 176 za mfuko wa
barabara kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati barabara, Milioni 168 za
mfuko wa Jimbo, na Milioni 307 za mfuko wa Afya (Busket Fund)
No comments:
Post a Comment