Thursday, May 19, 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI


'

JESHI LA MAGEREZA NCHINI LASAINI MKATABA WA UFUNDISHAJI ELIMU YA UJASILIAMALI KWA WAFUNGWA LEO DAR ES SALAAM


MIN1
MIN4Jeshi la Magereza limesaini Mkataba (MoU) na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Technoserve – Tanzania kushirikiana katika ufundishaji wa wafungwa mafunzo ya Ujasiriamali wakiwa wanakaribia kumaliza vifungo vyao magerezani ili stadi hizo ziwasaidie kumudu maisha mapya baada ya kutumikia adhabu zao.
Programu hii itaendeshwa katika Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mfuko wa “Master Card”  kwa vijana wa kike na kiume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 30 hivyo wafungwa walioko katika Magereza yaliyomo Mkoani humo na wengine wenye sifa toka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili kupata mafunzo kupitia progamu ya uimarishaji wa maendeleo ya vijana vijijini kupitia biashara “STRYDE” inayoendeshwa na Taasisi hiyo.
Takwimu za sasa zinaonesha kwamba kati ya asilimia 30 na 35 ya wafungwa wanaomaliza vifungo vyao hurejea magerezani.Hivyo, mafunzo haya yatalenga kuwafanya  wanapomaliza vifungo vyao waweze kupata maarifa ya kuanzisha shughuli zao wenyewe za kujipatia kipato halali na kuacha vitendo vya uhalifu katika jamii wanamoishi vinavyowafanya kurejea magerezani.
Aidha,  mafunzo haya ya Ujasiriamali yatajikita katika kuwafundisha kilimo biashara, matumizi mazuri ya fedha binafsi, uwezo wa kutumia ujuzi, ubunifu na tafakari ya kina katika kufanya maamuzi, mpango biashara, mawazo ya biashara na uwezo wa kuandaa mpango biashara n.k.
Ushirikiano huu ni mkakati endelevu wa Jeshi la Magereza katika kuboresha Programu za Urekebishaji wa wafungwa magerezani ili wawe raia wema na wenye tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Program za Ujasiriamali kwa wafungwa zinaendeshwa pia katika baadhi ya Magereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Dorcas International na New Life in Christ katika Gereza la Karanga – ushonaji viatu, ufumaji na uokaji mikate, Gereza Arusha – uokaji mikate, ufundi seremala na ufumaji.
Jeshi la Magereza linawakaribisha wadau wa ndani na nje kushirikiana katika urekebishaji wa tabia za wafungwa ili wawe na michango chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.

JESHI LA POLISI MWANZA LATOA BARAKA ZOTE ZA USALAMA KWA TAMASHA LA JEMBEKA 2016



Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha kubwa la Burudani JEMBEKA FESTIVAL 2016. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi Amewahakikishia Ulinzi na Usalama wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake pamoja na wageni wote watakao hudhuria tamasha la Jembeka festival 2016 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ya tarehe 21 Mei 2016 katika kiwanja Cha CCM Kirumba kilichopo jijini Mwanza.

Kamanda Msangi ameyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (Jembejembe) Alipomtembelea kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee nchini Tanzania.

“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza,wageni kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania hili ni tamasha la kipekee hapa mkoani kwetu hivyo napenda kuwaasa wananchi wote kufurahi na kuhudhulia tamasha hilo kwa furaha pia napenda kutoa rai kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa amani”,Alisema Kamanda Msangi.

Kwa upande wake Dr. Sebastian Ndege amemshukuru Kamanda Msangi kwa ushirikiano aliouonesha tangu awali na hili la sasa kuhakikisha anaimarisha ulinzi na usalama siku hiyo ya tamasha na kuahidi kutumia vyombo vyake vya habari katika kulisaidia jeshi hilo kutoa elimu ya ulinzi shirikishi.

“Nashukuru sana kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwa Jeshi la polisi ngazi zote kwani wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mwanza inakuwa salama hivyo mimi pamoja na timu yangu tunaahidi kusimama bega kwa bega na jeshi letu kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake stahiki linapokuja suala la ulinzi, usalama wa mtu mmoja mmoja na hata utoaji wa elimu kwa umma kuhusu namna ya kuzuia uhalifu, ili Mwanza yetu iwe mahali salama"

Aidha Kamanda Msangi ameahidi kuimarisha Ulinzi wa ndani na nje kwa maeneo yote ya wilaya ya Ilemela ambako uwanja wa CCM Kirumba ndiko unakopatikana na amewatoa hofu Wananchi wote pamoja na wageni watakaohudhuria tamasha hilo kwa kuhofia usalama. "Atakaye kuja kwa hila tutamdhibiti"

Tamasha la Jembeka festival 2016 mwaka huu litatumbuizwa na msanii kutoka nchi ya Marekani Neyo anayetarajiwa kutua nchini kesho usiku.Wakali wengine kutoka hapa nchini Tanzania akiwemo Diamond, Juma Nature, Ney wa Mitego, Maua Sama, Ruby, Fid q, Mo Music, Baraka da prince, na wengine kibao, wanatarajiwa kumwaga mvua ya burudani siku hiyo.

JEMBEKA FESTIVAL linaloandaliwa na Jembe ni Jembe Entertainment kupitia Jembe FM, hufanyika kila Mwaka mkoani Mwanza na tamasha hilo kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu sabini toka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Katibu wa Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee nchini Tanzania. 
Aksante sana Gazeti la Mwananchi toka Mwananchi Communication kwa kutusaidia kufikisha taarifa mlango kwa mlango PAMOJA SANA. 

Jumamosi hii, May 21,2016 itakuwa ni Jembeka Festival Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii wengine kibao. 

Kumbuka ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so huu ni muda wa kununua tiketi mwana wa kwetu.Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Mwananchi Communications,Samsung, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Binagi Blog, Michuzi Blog, Dj Choka, Lakairo Hotel na wadau wengine.

KATIBU MKUU UJENZI ATAKA TAARIFA NDANI YA SIKU MBILI UHARIBIFU WA FLOW METER NA CAMERA BANDARINI

FL1Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Hebel Mhanga( wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho( wa pili kulia) kuhusu ufanyaji kazi wa mifumo ya kuendesha mita ya kupimia mafuta (flow meter) uliojengwa eneo la Kwa Mwingira Mji Mwema Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na katibu Mkuu huyo leo Mei 18,2016.
FL2Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya (kulia) akitoa maelezo kwa  Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (kushoto) kuhusu mfumo wa kompyuta wa mita ya kupimia mafuta unavyofanya kazi kwa kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa wa utendaji kazi wa mita hiyo leo Mei 18,2016.
FL3Habour Master Kapteni Abdul Mwengamuno kutoka Mamalaka ya Bandari ya Dar es Salaam(kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (kushoto) hatua za kuzingatia wakati wa upakuaji wa mafuta kutoka kwenye meli mpaka kwenye mita za kupima mafuta ambapo mafuta hayo huchujwa kuondoa uchafu kwa kupitia mitambo maalum iliyofungwa kwenye mita hiyo.
FLO4Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho akipanda ngazi kuelekea kwenye pambu na valvu zilizofungwa kwenye mita ya kupimia mafuta(Flow Meter) wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utendaji kazi wa mita hiyo leo Mei 18,2016.
FLO5Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya(kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (wa pili kushoto) kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika moja ya valvu zilizoko kwenye  mita hiyo, upande unaoendeshwa  kwa kutumia  mfumo wa digitali  hali iliyosababishwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Mita hiyo sasa inatumia mfumo wa analojia na  hatua ya urejeshaji wa valvu hiyo katika hali yake ya awali inafanyiwa kazi na mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga mita hiyo leo.
FLO6Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho ( wa pili kulia) akitoa maagizo kwa Mamlaka ya Bandari kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ikiwemo hitilafu ya kamera za ulinzi na baadhi ya valvu kwenye mita ya kupimia mafuta na kuwasilisha taarifa ofisi kwake Jumatatu Mei 23 namna ya watakavyoshughulikia mapungufu yaliyojitokeza.
FLO7Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (mwenye Kaunda suti) kuhusu ufanyaji kazi wa mtambo unaochuja mafuta kwa lengo la kudhibiti na kuzuia mafuta machafu kuingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam leo Mei 18,2016.
FLO8Mita ya Kupimia Mafuta (Flow Meter) iliyojengwa eneo la kwa mwingira, mji Mwema Kigamboni  Jijini Dar es salaam . Utaratibu wa kujenga uzio na paa kufunika mtambo huo unaendelea kupitia mkandarasi aliyepewa jukumu la kujenga mradi huo ili kuhimarisha ulinzi na usalama wa mita hiyo.( Picha na Raymond Mushumbusi na Aron Msigwa -MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence- Maelezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Uchukuzi) Mhandisi Dkt. Leornad Chamuriho ameutaka uongozi wa Bandari unaosimamia Mitambo ya Kupimia Mafuta Nchini (Flow Meter) iliyoko Kigamboni kutoa taarifa ya kuharibika kwa mitambo hiyo ndani ya siku mbili.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika mitambo hiyo  na kubaini upungufu katika vitendea kazi ikiwemo kamera ya kufuatilia mwenendo bandarini hapo, “valvu, sloptank” na kuchelewashwa kwa ujenzi wa kufunikwa kwa mitambo.
“Ifikapo Jumatatu nipatiwe taarifa kuhusu matengenezo ya vifaa hivi, hatua zilizochukuliwa na mnieleze lini ukarabati wake utakamilika” alisema Dkt. Chamuriho.
Aidha, aliongeza kuwa dhumuni la Serikali ni kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya kazi ili kulinda mapato yatokanayo na mafuta yanayoingia nchini ili Serikali ipate kodi halali na hivyo kuongeza mapato ya nchi na kuondoa malalamiko kwa wateja.
Naye Meneja Mradi wa Mitambo ya Kupimia Mafuta kutoka Mamlaka ya  Bandari nchini Mhandisi Mary Mhayaya ameeleza kuwa uharibifu wa vifaa hivyo umesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na tayari vifaa hivyo vimeanza kufanyiwa kukabarati.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Hebel Mhanga amesema ofisi yake inajukumu la kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja wanaotumia mitambo hiyo iliyopo bandarini  hapo na Serikali inapata mapato kulingana na huduma iliyotolewa.
Mradi wa Mitambo ya Kupimia Mafuta nchini  ipo katika majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari meli tatu zimefanyiwa majaribio ya upakuaji wa mafuta huku moja ikiwa imefanyiwa vipimo.

MAJALIWA AKISALIMIANA NA VIONGOZI WA MKOA WA MOROGORO

MAJ1Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Morogoro wakati aliposimama kwa muda mfupi mjini hapo akiwa njiani kuelekea Dodoma akitoka Dar es salaam May 18, 2016. Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Dk. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAJ2

NSSF YATOA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA

Shirika la  Taifa la  Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni  mpango maalamu wa kuwafikia wanachama  wengi zaidi.
 
Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero. Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
Afisa Masoko na Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha. 
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.
Afisa wa NSSF Bi. Irene Mshanga akimwandikisha mwanachama Mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika soko la Kilombero jijini Arusha.
 Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amina
Mbaga Akitoa ufafanuzi kwa Mwanchama mpya wakati wa Kampeni maalumu ya
kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika Soko la Kilombero Jijini
Arusha leo.
Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Anna Nguzo Akitoa
ufafanuzi kwa Mwanchama mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama
wengi zaidi inayoendelea katika Soko la Kilombero Jijini Arusha leo.

TFDA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA WADAU KUHUSU USALAMA WA CHAKULA BARANI AFRIKA


Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, akitoa maelezo ya awali katika ufunguzi wa mafunzo kwa washiriki wa Kongamano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Bara la Afrika. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (aliyekaa
katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya siku
tano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Afrika.
Wengine waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi
wa Huduma za Maabara wa TFDA, Bi. Charys Ugullum, Mwakilishi wa FAO na
Mwakilishi wa IAEA, Bw. Alex Mulori. 
 
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa mwenyeji wa mafunzo ya siku tano, tarehe 16 – 20 Mei, 2016, kwa wadau wa udhibiti katika mnyororo wa Usalama wa Chakula hususan upimaji katika maabara Barani Afrika. 
Akifungua mafunzo hayo yaliyowashirikisha wadau wapatao 50 kutoka nchi 15 za Afrika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, alisema kuwa Lengo kuu la mafunzo na mkutano ni kujadili majukumu, wajibu na mchango wa kila mdau katika suala zima la kuhakikisha chakula ni salama kwa walaji. 

Dr. Mpoki alisema, “ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa wa namna bora ya usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa Chakula Salama kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau mliopo hapa’ . 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, wakati wa kutoa maelezo ya awali kuhusu mafunzo hayo yanayodhaminiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Nguvu za mionzi (IAEA), alieleza kuwa kufanyika kwa mafunzo haya nchini Tanzania ni heshima kubwa na ishara ya mwendelezo wa TFDA kufikia Dira yake ya kuwa taasisi inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa Tiba. 
Nchi zinazoshiriki katika mafunzo haya ni pamoja na Algeria, Benin, Botswana, Cameroon, Egypt, Ethiopia, Mauritius, Mali, Chadi, Namibia, Sudan, Tunisia, Uganda, Zimbabwe na Tanzania.Matokeo ya mafunzo haya yatakuwa ni dira ya utekelezaji wa mradi wa udhibiti wa mnyororo wa Usalama wa Chakula kabla ya kufikia mwisho wa mwezi Disemba 2016. Wadau wa mnyororo wa udhibiti wa Usalama wa Chakula walioshiriki katika mafunzo haya wanatoka kwenye maeneo ya maabara, ukaguzi, uzalishaji wa vyakula na walaji.