Tuesday, May 3, 2016

MAAZIMISHO YA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ DUNIANI YAFANA



Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na wadau wa Sanaa kwenye maadhimisho ya Siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika mapema wiki hii katika Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijinI Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Msanii mkongwe John Kitime na Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Mareges.
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Maximilan Chami akitoa elimu kwa wasanii na wadau wa Sanaa kuhusu maadhimisho ya siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko ofisi za Baraza hilo Ilala Sharif Shamba. Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza.
Msanii mkongwe na mchambuzi wa masuala ya Sanaa John Kitime akifafanua juu ya kwa nini bendi nyingi nchini zilitumia jina la jazz wakati akiwasilisha mada kwenye maadhimisho ya siku ya muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Mwakilishi kutoka UNESCO Maximilan Chami na Afisa Habari wa BASATA Aristides Kwizela.
Msanii Mkongwe wa muziki wa reggae na mchambuzi wa masuala ya Sanaa Innocent Nganyagwa (Katikati) akiimba sambamba na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (Kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Mareges kwenye maadhimisho ya siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaongoza zaidi ya wasanii na wadau wa Sanaa mia moja katika maadhimisho ya siku ya Jazz duniani yaliyofanyika makao makuu ya Baraza hilo yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Maazimisho hayo ambayo yameazimishwa kwa mara ya kwanza nchini yalipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Bendi ya muziki wa Jazz huku wataalam na wasanii wakongwe wakiwasilisha mada mbalimbali katika kongamano maalum lililobeba mijadala na hoja mbalimbali kuhusu muziki huo.

No comments:

Post a Comment