Washindi wa shindano la bahati Nasibu la Fiesta condoms Bw & Bi. Justin Tinieshimo wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma. Washindi hao waliweza kufurahia siku saba za mapumziko mjini Dubai katika safari iliyodhaminiwa na Shirika la DKT Tanzania katika kutekeleza ahadi ya ushindi wao wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa Chapa mpya ya “Fiesta condoms” miezi miwili iliyopita Ledger Plaza hotel jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa shirika la DKT Tanzania Bi. Hellen Kimati akitoa zawadi ya shada la maua kwa washindi wa shindano la bahati nasibu la Fiesta condoms Bw & Bi. Justin Tinieshimo mara baada ya wageni hao kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma.
Mshindi wa shindano la bahati nasibu Bi. Gloria Tinieshimo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili akitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma. (Kulia) ni mume wake Bw. Justin Tinieshimo ambaye aliongozana naye katika safari hiyo ya wiki nzima iliyodhaminiwa na shirika la DKT Tanzania mara baada ya wawili hao kuibuka washindi wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa chapa ya Fiesta condoms miezi miwili iliyopita Ledger Plaza hotel jijini Dar es salaam.
KATIKA jitihada za kutangaza matumizi ya njia za uzazi wa mpango na kuzuia mimba zisizotarajiwa na magonjwa yanayo ambukizwa kwa kujamiiana (STDs) nchini, miezi miwili iliyopita katika siku ya wapendanao (valentine day), DKT International Tanzania shirika lisilo la kiserikali ambalo ni moja kati ya watoaji wakubwa wa bidhaa za uzazi wa mpango na afya ya uzazi nchini ilifanya uzinduzi wa aina mbalimbali za kondom zenye ubora zilizopewa jina la “Fiesta kondom” huko Bahari Beach Ledger Plaza hotel, Dar es salaam.
Wakati wa uzinduzi, shindano la bahati nasibu lilifanyika ambapo wanandoa watatu walishinda safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda na kurudi Zanzibar, Afrika ya kusini na Dubai.
No comments:
Post a Comment